Ushauri wa Kisheria
Ushauri wa Kisheria
Huduma hii inakuunganisha na wanasheria wenye uzoefu katika sekta ya ujenzi, ili kutoa ushauri wa kisheria kwa miradi yako. Huduma hii inahusisha kuunganishwa na wanasheria wa kuaminika ambao wataweza kutoa ushauri kuhusu mikataba, leseni, haki za ardhi, na taratibu za kisheria zinazohusiana na ujenzi.
Mteja atapata huduma hii kwa kupitia jukwaa letu, ambapo atachagua aina ya huduma ya kisheria anayotaka, kisha tutamuwezesha kuwasiliana na mshauri wa kisheria anayeafiki mahitaji yake. Huduma itatolewa kwa njia ya ushauri wa moja kwa moja, kwa njia ya simu, barua pepe, au mikutano ya ana kwa ana, kulingana na makubaliano kati ya pande hizo.
Huduma ya ushauri wa kisheria inapatikana kwa gharama ya TZS 150,000 kwa lisaa. Malipo hufanyika baada ya huduma ya ushauri kutolewa, na mteja atakuwa na uhuru wa kulipa baada ya kukamilika kwa kikao cha ushauri.
Sambaza
Haikuweza kupakia upatikanaji wa kuchukua
